Mwanamuziki wa Marekani, Robyn Fenty maarufu kama Rihanna ameishtua dunia kwa kuweka rekodi ya kuwa mwanamuziki wa kike aliyekuwa ‘bilionea’ kwa kiwango cha dola za Marekani.

Jarida la Forbes jana lilimtaja Rihanna kuwa amefikisha kiwango cha utajiri cha $1.7 bilioni, kiwango ambacho hakijafikiwa na mwanamuziki yeyote wa kike.

Kiwango hicho cha utajiri ni cha juu zaidi ya tajiri namba moja wa Tanzania, Mohammed Dewji ambaye Jarida la Forbes linamkadiria kuwa na utajiri wa $1.6 bilioni kwa mwaka 2021.

Aidha, Rihanna ameshika nafasi ya pili nyuma ya Oprah Winfrey, wakiwa ndio wanawake matajiri zaidi kwenye kiwanda cha burudani duniani.

Mwanamuziki huyo ameingiza fedha nyingi zaidi kupitia biashara zinazomlipa kwa jina la muziki na sio muziki moja kwa moja. Ikizingatiwa kuwa ni miaka mitano tangu alipoachia albam yake ya mwisho ‘Anti’, ambayo ilikaa kwenye ‘charts’ za Billboard kwa takribani wiki 63.

Dili: Wanaopata chanjo ya corona kulipwa Sh. 2,300,000

Rihanna amewekeza zaidi muda kwake kwenye biashara yake ya urembo na amefanikiwa kutusua kwelikweli kupitia ‘Fenty Beauty makeup line’.

Forbes wamekadiria kuwa biashara ya Fenty Beauty pekee ina thamani ya $2.8 bilioni. Katika kipindi cha mwaka 2018, biashara hiyo ilikuwa inatengeneza kiasi cha $550 milioni kwa mwaka.

Imeelezwa kuwa siri ya mafanikio ya biashara ya Rihanna ni kuhakikisha inakuwa kwa ajili ya wanawake wa aina zote, wenye maumbe na aina mbalimbali za ngozi.

“Alikuwa na biashara ambayo ilikuja na kusema ‘ninataka kuongea na kila mwanamke mwenye aina yoyote. Wanawake wengi walijisikia kama hakuna mpaka wa kutumia bidhaa za Fenty Beauty, ikiwa ni ngozi nyeupe, nyeusi na za kati,” Forbes inamkariri Coyne.

Mawaziri wa Afya Tanzania,Kenya kukutana leo
Pascal Msindo atimkia Uturuki