Mwanamuziki Robyn Rihanna Fenty maarufu Rihanna ametunukiwa cheti cha heshima kama shujaa wa taifa la Barbados ‘National Hero of Barbados”.

Rihanna ametunukiwa wadhifa huo kwenye hafla maalumu ya kuondoka kwa utawala wa Malkia Elizath II wa Uingereza.

Hafla hiyo imefanyika usiku wa kuamkia leo Nov 30, 2021 Mbele ya Rais mpya wa nchi hiyo Sandra Mason.

Licha ya kuwa ni msanii mwenye mafanikio na heshima kubwa Duniani kote, kwa sasa Rihanna amepachikwa wadhifa wa kitaifa unaompa dhamana ya kuitwa Mheshimiwa.

Rihanna anaingia kwenye orodha ya mashujaa wasio pungua kumi na moja (11) katika historia ya taifa hilo, huku akitajwa kama mtu wa kwanza kutunukiwa tangu mwaka 1998.

Pamoja na kuipeperusha vyema bendera ya Barbados, inaelezwa miongoni mwa chachu iliyopelekea Rihanna kupewa wadhifa huo ni kutokana na kuonyesha kupaza sauti kwa kuinadi nguvu zote Barbados na vivutio mbali mbali vinavyopatikana katika taifa hilo, akiwa kama balozi wa Utalii.

Pablo: Morrison atatusaidia sana
Waziri Nchemba aongoza kikao kazi cha EAC