Vipimo vya kupimia ujauzito Zanzibar vimebainika kuwa na mapungufu baada ya kudaiwa kubaini mimba kwa baadhi ya wanaume waliofanya vipimo katika moja ya Hospitali ya Serikali Visiwani humo.

Hayo yamebainishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar – CAG, Dkt. Othman Abbasi Ali wakati akiwasilisha ripoti ya fedha kwa mwaka wa 2021/2022 Ikulu mjini Unguja.

Ripoti hiyo iliyosomwa mbele ya Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi pia imeibua uwepo wa dawa zenye thamani ya shilingi bilioni 3.3 ambazo si salama kwa matumizi ya binadamu.

Aidha, ripoti hiyo pia imeeleza kuwa Bohari Kuu ya Serikali imekuwa ikisambaza dawa ambazo zimeisha muda wake wa matumizi.

Fiston Mayele: Hatukuwa na bahati ya ubingwa
Asilimia 70 ya taka Baharini ni plastiki - Dkt. Mpango