Hatimaye Kamati ya Taifa ya Kuwalinda Tembo na Faru imetekeleza agizo la Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa kwa kumkabidhi ripoti rasmi ya uhamisho na kifo cha faru aliyepewa jina la John.

Akisoma taarifa hiyo leo nyumbani kwa Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alisema kuwa Desemba mwaka jana Faru John alihamishwa kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko katika Hifadhi ya Gurumeti.

Alisema kuwa hadi faru huyo anahamishwa alikuwa na watoto 26 ambao ni sawa na asilimia 70.2 ya faru wote waliokuwepo.

Aidha, Profesa Maghembe alisema uamuzi wa kumhamisha faru huyo ulilenga kupunguza tatizo la ‘inbreeding’ kwa lengo la kuwaokoa faru weusi kwenye hifadhi hiyo.

Kwa mujibu wa Waziri Maghembe, baada ya kumhamisha, afya ya faru John ilianza kuzorota Julai 10 mwaka huu na alifariki Agosti 18 mwaka huu.

Desemba 6 mwaka huu, akiwa Mkoani Arusha, Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa hifadhi hiyo kuhakikisha wanawasilisha nyaraka zote zilizotumika kumhamisha Faru John ifikapo Desemba 8 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, alipokea taarifa hiyo majira ya saa 7 usiku wa kuamkia leo.

Waziri Mkuu apokea taarifa za Faru John, ataka uchunguzi zaidi
Some tips on crafting a reliable research paper produce educational essays