Uchumi wa Tanzania unategemea kukua kwa asilimia 5.2 mwaka huu wakati ambapo nchi nyingine sita za Mashariki mwa Bara la Afrika zikitarajia kuporomoka kiuchumi kwa sababu ya athari za janga la corona.

Kiwango hicho cha ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni zaidi ya nchi zote za Mashariki mwa Bara la Afrika, kwa mujibu wa Ripoti ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Hata hivyo, kabla ya kutokea kwa mlipuko wa virusi vya corona, AfDB ilitarajia kiwango cha uchumi wa Tanzania kukua kwa asilimia 6.4.

Nchi sita za Mashariki mwa Bara la Afrika ambazo kiwango chao cha uchumi kimeporomoka zaidi ni Seychelles (-10.5), Sudan (-7.2), Burundi (-5.2), Somalia (-3.3), Comoro (-1.2) na Sudani Kusini (-0.4).

Nchi nyingine sita ambazo uchumi wake utakuwa lakini ziko chini ya kiwango cha wastani wa ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa mwaka huu ni Rwanda (4.2), Ethiopia (3.1), Uganda (2.5), Kenya (1.4), Djibouti (1) na Eritrea (0.3).

AfDB imeeleza kuwa pato la ndani la Tanzania (GDP) litawezeshwa zaidi na ongezeko la bei ya dhahabu iuzwayo nje ya nchi.

Ripoti ya mwezi Mei inaonesha kuwa dhahabu imeongoza kwa kuingiza fedha nyingi zaidi za kigeni Tanzania, ikizidi sekta ya utalii ambayo ilikuwa ikiongoza kabla ya mlipuko wa corona.  

Mazingiza: Haturudii makosa ya kupoteza mchezo wa 'DABI'
Luc Eymael: Ni mchezo muhimu sana kwetu