Wiki chache baada ya mkutano kati ya Rais Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un kuvunjika, ripoti zimeeleza kuwa maandalizi ya majaribio ya makombora ya nyuklia yameanza.

Kwa mujibu wa ripoti za kiintelijensia za Korea Kusini inayoshirikiana na Marekani, Korea Kaskazini wameendelea kuandaa eneo la Sanumdong  lililo karibu na Pyongyang kwa ajili ya kuzindua tena majaribio hayo.

Trump ameeleza kuwa kama taarifa hizo zitakuwa za kweli, watakuwa wamemuangusha kutokana na hatua ambayo walikuwa wameshaipiga ya kufanya mazungumzo na kukubaliana kusitisha majaribio hayo.

“Nitavunjika moyo na itanishangaza kama Kim atafanya chochote ambacho hakiendani na tunachokifahamu, lakini tutaona nini kinatokea,” alisema.

Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wanadai kuwa katika hatua waliyoifikia huenda wanajiandaa kuzindua satellite na sio makombora ya nyuklia.

Mkutano kati ya Trump na Kim Jong Un uliokuwa unafanyika nchini Vietnam ulivunjika baada ya wawili hao kutokubaliana katika masuala ya msingi. Kim alitaka vikwazo dhidi ya nchi hiyo viondolewe kama sharti la wao kuteketeza baadhi ya vinu vya makombora ya nyuklia, lakini Trump alisema hawakuwa wamejiandaa kwa hilo.

Mkutano huo ulikuwa wa pili kati ya viongozi hao baada ya ule wa Singapole.

Jela miaka 11 kwa kumkeketa mwanaye jijini London
Video: Sasa ni Lowassa vs Chadema, Kibonde kuzikwa alipolala mkewe

Comments

comments