Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi wa tukio la moto uliotokea katika soko la kimataifa la Kariakoo Julai 10, 2021 jijini Dar es salaam nakupelekea baadhi ya wafanyabiashara kupoteza mali zao.

Amepokea taarifa hiyo kutoka kwa Mwenyekiti Kamati hiyo, CP Liberatus Sabas na kuahidi kuwa Serikali itayafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati hiyo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewashukuru na amewapongeza wajumbe wa kamati hiyo kwa kazi nzuri iliyofanyika kwa weledi mkubwa ambapo amesema ataifikisha taarifa hiyo kwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwani tukio hilo limewagusa watu ndani na nje ya nchi.

“Naahidi mbele yako mwenyekiti kuwa Serikali nimeridhishwa na taarifa mliyo nikabidhi leo na mapendekezo yote mliyoyatoa yatazingatiwa” amesema Majaliwa

Itakumbukwa Julai 11, 2021 Majaliwa alitembelea na kukagua hatua zinazoendelea kuchukuliwa kudhibiti moto katika soko la kimataifa la Kariakoo na kutangaza kamati ambayo ilipewa kazi ya kuchunguza tukio hilo ili kubaini chanzo cha moto huo.

Serikali mpya Lebanon kuundwa na Waziri mkuu wa Zamani
Mradi huu ukamilike mapema- Makamu wa Pili Rais