Ripoti ya Utafiti ya utumikishwaji watoto ya mwaka 2014/15 imezinduliwa leo na Ofisi ya taifa ya takwimu jijini Dar es salaamu,kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali yanayotetea haki za watoto duniani na kuhudhuliwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu sera,bunge,kazi,ajira,vijana wenye ulemavu Mh.Abdallah Possy mapema hii leo.

Ofisi ya takwimu kupitia kwa mkurugenzi wake Dkt Albina Chuwa alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya takwimu ya mwaka 2015 unaipa mamlaka ofisi hiyo kuratibu na kusimamia  utoaji wa takwimu rasmi nchini.

Aidha aliongeza kuwa lengo  la utafiti huo ni kutaka  kujua hali ya watoto wanaofanya kazi za kiuchumi  na zisizo za kiuchumi,utumikishwaji wa watoto kwenye kazi na mzingira hatarishi na athari mbalimbali zinazo wapata za kiafya,kisaikolojia na mahudhurio mabaya mashuleni.

Lengo la ofisi ya taifa ya takwimu ni kuhakikisha serikali na wadau wengine wanapata taarifa kila robo mwaka hivyo (NBS)wameanza kutengeneza mfumo ujulikanao kama ‘’e-population register’’ambao utzinduliwa hivi karibuni kwa lengo la kuhakikisha zinzpatikana’’alisema Dkt.Chuwa.

Utumikishwaji watoto (Child Labour)umekua ni tatizo  kubwa duniani kote ambapo  asilimia 11(watoto milioni 264)wenye umri wa miaka 5-17 wanatumikishwa kwenye ajira mbalimbali ambapo hizi ni takwimu za makadirio ya watoto tangu mwaka 2000-2012 za shirika la kazi Duniani ILO.

Kwa upande wa Tanzania,utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014/15 yanaonesha kuwa  kati ya watoto milioni 15 wenye umri kati ya miaka 5 hadi 17,watoto milioni 4.2 sawa na asilimia 28.8 wanatumikishwa katika kazi mbalimbali za kiuchumi,sekta ya kilimo,misitu, na uvuvi inaongoza kwa kiwango cha asilimia 92.1 ya watoto wanaishi vijijini.na kauli mbiu ilikua ni ‘’WEKEZA KWA KIJANA WA KIKE’’

Hata hivyo kwa upande wake mgeni rasmi Mh,Abdallah possy alitoa wito kwa watanzania kubadilisha mitazamo na malengo pia mfumo wa maisha na kusema serikali itaendelea kupambana na utumikishwaji pia aliwatka wazazi kuwapeleka watoto wao shule.

Tanzania Yapata Tuzo Mkutano AU
Ole Milya Awataka Bavicha Kuenzi Mienendo ya Nyerere na Mandela