Mtaalamu maalumu wa sheria kutoka Umoja wa Mataifa anayechunguza mauaji ya mwandishi habari wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi amependekeza ufanyike uchunguzi juu ya uwezekano wa ushiriki wa mwanamfalme Mohammed bin Salman katika mauaji hayo.

Mwanasheria huyo amesema kuwa upo ushahidi wa kuaminika unaomhusisha mrithi huyo wa ufalme na mauaji hayo.

Madai kuhusu uwezekano wa jukumu la moja kwa moja la mrithi wa kiti cha ufalme, Mohammed bin Salman katika mauaji ya Khashoggi yaliyotokea Oktoba mwaka jana yamebainishwa kwa kina katika ripoti mpya ya mchunguzi maalumu kuhusu mauaji ya kinyume cha sheria, Agnes Callamard.

Hata hivyo, ripoti hiyo yanye kurasa 101 juu ya mauaji ya Khashoggi kwenye ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul nchini Uturuki, inatoa mwito kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa au Katibu Mkuu Antonio Guterres, kufungua uchunguzi zaidi wa uhalifu.

LIVE: Yanayojiri bungeni jijini Dodoma
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 20, 2019