Watu wawili wameuawa, na wengine 15 kujeruhiwa wakati wajumbe wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO) katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), walipofyatua risasi kwenye kituo cha mpakani eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Serikali ya Kongo, tukio hilo lilitokea Jumapili Julai 31, 2022 katika eneo la Beni nchini DRC, wakati wanajeshi wa kikosi cha MONUSCO wakivuka na kuingia nchini humo kutokea Uganda.

Video iliyosambaa kwenye mitadao ya kijamii, imemuonesha mwanaume mmoja aliyevalia sare za Polisi na mwingine aliyevalia sare za Jeshi wakisonga mbele kuelekea kwenye msafara wa Umoja wa Mataifa.

Wanajeshi wa kulinda amani

Baada ya kurushiana maneno, walinzi wa amani walionekana kufyatua risasi kabla ya kufungua geti, kuendesha gari na kuendelea kufyatua risasi huku watu wakitawanyika au kujificha.

“Wakati wa tukio hili, askari wa kikosi cha uingiliaji kati cha MONUSCO waliokuwa wakirejea kutoka likizo walifyatua risasi kwenye kituo cha mpakani kwa sababu zisizoeleweka na kulazimisha kupita,” ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Kasindi ulisema katika taarifa siku yake.

Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema amekasirishwa na tukio hilo na kudai uwajibikaji unahitajika ili kuweka mambo sawa na kwamba hiyo ni fedheha kusikia wanachama wa kitengo cha kulinda amani, taarifa ya Umoja wa Mataifa wanarushiana risasi.

Bien wa Sauti Sol aonyesha jeuri ya pesa
Mafuriko yauwa tisa baada ya Mito yapasua kingo