Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya klabu ya Rivers United Charles Mayuku amethibitisha taarifa za kufika salama kwa kikosi chao nchini Nigeria, baada ya kuondoka mapema jana Jumatatu (Septemba 13) jijini Dar es salaam.

Rivers United walikuja nchini juma lililopita kwa ajili ya mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya awali dhidi ya Young Africans uliocheza Jumapili (Septemba 12), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijii Dar es salaam.

Mayuku ambaye alidai kufanyiwa fujo wakati wa mchezo dhidi ya Young Africans, amesema baada ya kuwasili nchini Nigeria kikosi chao kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Enyimba FC, ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na mpambano wa mkondo wa pili dhidi ya Young Africans.

“Tumefika salama nyumbani na leo au kesho tunatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Enyimba FC, naamini utatusaidia kabla ya kukutana na Young Africans Jumapili hapa Nigeria.

Kuhusu wachezaji na viongozi waliodaiwa kukutwa na maambukizi ya Corona, Mayuku amesema: “Wachezaji wetu (4) na viongozi (3) waliokutwa na Corona wako salama na hakuna mwenye maambukizi, nadhani zilikuwa mbinu chafu za wapinzani wetu.”

“Bado wageni wetu (Young Africans ) hawajatupa taarifa ni lini wanatarajia kuwasili nchini (Nigeria), lakini tumejipanga kuwapokea kama walivyotupokea.”

Rivers United wanaongoza kwa ushindi wa bao 1-0 walioupata Jumapili (Septamba 12) Uwanja wa ugenini jijini Dar es salaam, na watalazimika kuulinda ushindi huo ama kuongeza ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya kwanza ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Mbombo: Nitafunga sana 2021/22
Luis Miquissone aahidi makubwa Al Ahly