Hatimaye kiungo mshambuliaji wa klabu bingwa nchini England, Leicester City, Riyad Mahrez amevunja ukimya na kueleza mustakabali wake, baada ya kuwa sehemu ya kikosi kilichopata mafanikio klabuni hapo.

Mahrez, amelazimika kuvunja ukimya baada ya kuchoshwa na taarifa zilizokua zikiandika kila leo kuhusu mustakabli wake, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kisoka, ambao ulisaidia kufikia lengo la Leicester City kuibuka mabingwa msimu wa 2015-16.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, amesema hana mpango wa kuondoka klabuni hapo na amekua akishangazwa na taarifa za kuhusishwa na mipango ya kujiunga na baadhi ya klabu za nchini England na nje ya nchi hiyo.

The Algeria forward celebrates with his family after a stunning season

Riyad Mahrez akisheherekea na familia yake dakika chache baada ya timu ya Leicester City kukabidhiwa kombe la ubingwa wa EPL siku ya jumamosi.

Mahrez ambaye alitajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka katika tuzo za chama cha wachezaji wa kulipwa nchini England (PFA), ameongeza kwamba hajali yanayozungumzwa dhidi yake, lakini amesisitiza kwamba yeye ndio mwenye kufanya maamuzi na ameshatangaza ataendelea kubaki King Power Stadium.

“Ninafuraha ya kuendelea kuwepo hapa, ninajivunia kuwa hapa na kutwaa ubingwa wa ligi ya England, na kwangu limekua jambo kubwa.” Alisema Mahrez aliyesajiliwa na Leicester City kwa ada ya uhamisho wa Pauni 400,000 akitokea Le Havre ya nchini Ufaransa mwaka 2014.

Tangu alipojiunga na klabu hiyo iliyotwaa ubingwa wa England kwa mara ya kwanza msimu wa 2015-16, Riyad Mahrez amefanikiwa kucheza michezo 86 na kufunga mabao 25.

Chadema waanza kushikana Uchawi
Danny Welbeck Amuweka Majaribuni Roy Hodgson