Vinara wa ligi kuu ya soka nchini England, Leicester City huenda wakampoteza mshambuliaji wao wa pembeni kutoka nchini Algeria, Riyad Mahrez, itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Mahrez, ambaye amekua na usaidizi mkubwa katika mafanikio ya klabu ya Leicester City, msimu huu anahusishwa na taarifa za kuwa kwenye mipango ya mabingwa wa soka barani Ulaya FC Barcelona.

Meneja wa Barca, Luis Enrique ameonekana kuwa mstari wa mbele kushinikiza Mahrez, asajiliwe kikosini mwake kwa msimu ujao wa ligi, kutokana na kuridhishwa na uwezo na ufanisi wa kazi zake kwa msimu huu.

Hata hivyo wadadisi wa masuala ya soka barani Ulaya wanahisi huenda pakaibuka vita kubwa ya kuwaniwa kwa Mahrez, itakapofika mwishoni mwa msimu huu, kutokana na klabu kadhaa kuwa katika mipango kama ya FC Barcelona.

Taarifa zinasema kwamba Enrique amemuangalia sana mchezaji huyu mwenye miaka umri wa miaka 25 na kuvutiwa sana na aina yake ya kufunga.

Lakini hata hivyo baadhi ya wadadisi hao wamekinguuka na kueleza mitazamo yao inayotaka kufanana kwa kusema itakua rahisi kwa FC Barcelona kumpata Mahrez, kutokana na mafanikio waliyojizolea kwa miaka ya hivi karibuni.

Imeelezwa kwamba hakuna mchezaji asiyependa kucheza na kikosi kinachoshinda mataji kama FC Barcelona, hivyo kutakua na hamu kubwa kwa Mahrez kutaka kujiunga na kikosi hicho ambapo atafaidika kiuchumi na kimchezo pia.

Azam FC Kusafiri Kesho Kuelekea Afrika Kusini
Mkwasa Atangaza Kikosi Cha Taifa Stars