Kiungo mshambuliaji kutoka nchini Algeria Riyad Mahrez, amefunguka kuhusu kukwamishwa kwake kujiunga na klabu ya Arsenal kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.

Kiungo huyo wa klabu bingwa nchini Uingereza (Leicester City), amesema alikua tayari kuelekea kaskazini mwa jijini London lakini uongozi wa The Foxes ulikataa kukutana na upande wa pili kwa ajili ya mazungumzo.

Mahrez amedai kuwa, meneja wa Leicester City Claudio Ranieri, alikua kikwazo kikubwa katika mpango huo kwa kusudio la kutaka kumtumia kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya pamoja na ligi ya Uingereza (PL).

“Kulikua na dalili zote za kujiunga Arsenal, Lakini Leicester walifanya kila njia za kunibakisha King Power Stadium na bado kwangu niliona kuna haja ya kuheshimu uamuzi huo.

“Sikutaka kulazimika suala la uhamisho wangu kuelekea kwingine, kwa sababu nilijua ningeweza kuibua matatizo na viongozi.

“Kwangu mimi bado naamini maamuzi ya kuendelea kubaki Leicester City bado ni sahihi.

“Ni wakati mwingine kwangu kuonyesha uwezo wangu kwa kushirikiana na wengine kuisaidia Leicester City kupata mafanikio kwa msimu huu.” Mahrez aliiambia tovuti ya Canal Football Club.

Rais Magufuli apokea hati za utambulisho za Balozi wa Sudan, Slovakia, Ukraine na Ghana
Video: Kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni uendelezaji Makao Makuu Dodoma - Majaliwa.