Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich, Robert Lewandowski ameomba kuondoka katika klabu hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka minne.

Lewandowski mwenye umri wa miaka 29 ana mkataba unaomtaka kubaki katika klabu hiyo mpaka mwaka 2021 lakini wakala wake wa sasa Pini Zahavi amesema mshambuliaji huyo anatamani kuondoka Bayern Munich kutafuta changamoto mpya.

Itakumbukwa kuwa Pini Zahavi ndiye aliyefanikisha uhamisho wa rekodi ya Dunia wa Neymar kwenda PSG na upo uwezekano wa wakala huyo kufanikisha dili ya Lewandowski kwenda katika vilabu kama Real Madrid, Chesea, PSG na Man Utd ambavyo vimekuwa vikimuwania.

Mshambuliaji huyo raia wa Poland amefunga mabao 151 katika mechi 195 tangu alipojiunga na Batern Munich mwaka 2014 akitokea Borrusia Dortimund kwa uhamisho huru.

Jeshi la Polisi sasa kusimamia usafi mitaani
Mkosoaji wa Serikali ya Urusi auawa kwa kupigwa risasi

Comments

comments