Hatimaye Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amerejea jijini Dar es salaam, akitokea nchini kwao Brazil alikokwenda kwa ajili ya kushughulikia changamoto ya kifamilia.

‘Robertinho’ amewasili jijini humo mapema leo Jumatano (Februari Mosi) majira ya alfajiri, na kupata mapokezi kutoka kwa maafisa wa Simba SC.

Baada ya kuwasili Kocha huyo alionekana mwenye furaha, huku akizungumza mawili matatu na maafisa waliofika kumpokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Kurejea kwa Kocha ‘Robertinho’ kunamaanisha atakuwa sehemu ya benchi la Ufundi keshokutwa Ijumaa (Februari 03), wakati wa mchezo wa Mzunguuko wa 23 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Stars.

Robertinho aliondoka nchini baada ya mchezo wa Mzunguuko wa 22 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Dodoma Jiji FC, ulioshuhudia Simba SC ikichomoza na ushindi wa 1-0 jijini Dodoma, huku akikosa mchezo wa Kombe la Shirikisho Hatua ya 32 Bora dhidi ya Coastal Union.

Usajili wa Hakim Ziyech wakwama
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 1, 2023