Kocha Mkuu wa Simba C Roberto Oliviera ‘Robertinho’, amempigia Saluti Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama kwa kiwango kizuri alichokionesha dhidi ya Singida Big Stars na Al Hilal ya Sudan.

Chama alikuwa sehemu ya wachezaji waliochagiza ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Singida Big Stars Ijumaa (Februari 03), huku akisaidia matokeo ya sare ya 1-1 dhidi ya Al Hilal jana Jumapili (Februari 05), Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kocha Robertinho amesema Chama ni mchezaji mzuri mwenye maarifa na kwenye michezo hiyo amecheza katika kiwango cha juu sana, akiwa nguzo imara ya mafanikio ya kikosi chake.

“Unataka kujua kuhusu Chama alichokifanya, jibu langu litakuwa ni maajabu, amefanya kitu ambacho mimi nataka.”

“Amecheza vizuri sana, Chama ni mchezaji mzuri, unaweza kuona akiwa na mpira mguuni mwake, anakua ni mtu mwenye kufanya maamuzi ya haraka kwa ajili ya kuisaidia timu kupata ushindi.”

“Watu wengi hawakunielewa mwanzoni, lakini kwa sasa watakuwa wameelewa, nilihiji mchezaji kama Chama acheze vipi katika kikosi changu, kwa hakika hivi ndivyo ninavyotaka Chama acheze kwa maslahi ya timu na ushindi wetu.” amesema Kocha Robertinho

Katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Al Hilal, Chama aliingia kipindi cha pili, na kusaidia Simba SC kupata bao la kusawazisha lililofungwa na Habib Kyombo.

CCM haikushinda uchaguzi 2020: Lissu
Burna Boy apigwa chini tuzo za GRAMMY 2023 Tems aibuka kinara