Uongozi wa klabu ya Aston Villa, unatarajiwa kumtangaza meneja kutoka nchini Italia Roberto Di Matteo, ndani ya saa 48, baada ya kumaliza taratibu za mazungumzo ya kumpa ajira.

Mwenyekiti wa Aston villa ambayo msimu ujao itashiriki ligi daraja la kwanza nchini England, Steve Hollis amethibitisha kukutana na Di Matteo na kufanya mazungumzo ya mwisho kabla ya kumtangaza mbele ya waandishi wa habari.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti la SunSport la nchini Engalnd, umebaini kwamba mazungumzo ya mwisho kati ya pande hizo mbili yalikamilika mwishoni mwa juma lililopita na Di Matteo amekubali kupokea mshahara wa Pauni 35,000 kwa juma.

Makubaliano hayo yameshapatiwa baraka na mmiliki wa Aston Villa Tony Xia, ambaye amedhamiria kuona klabu hiyo ikipambana vilivyo msimu ujao na kufankisha azma ya kurejea ligi kuu katika msimu wa 2017-18.

Mameneja wengine ambao walikua wakihusishwa na mpango wa kutaka kuajiriwa na klabu ya Aston Villa ni Nigel Pearson pamoja na David Moyes.

Man Utd Ya Jose Mourinho Kuanza Na Paul Pogba
Jurgen Klopp Kumfungulia Milango Pepe Reina