Mshambuliaji kutoka nchini Brazil Roberto Firmino Barbosa de Oliveira (Roberto Firmino), amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya Liverpool ambayo ilimsajili mwaka 2015 akitikea 1899 Hoffenheim ya Ujerumani kwa ada ya Pauni milioni 29.

Mshambuliaji huyo ambaye tayari ameshaifungia Liverpool mabao 27 katika michuano yote aliyocheza msimu huu, amefikia maamuzi ya kukubali kusaini mkataba huo, baada ya kukamilisha mazungumzo na viongozi wa juu huko Anfield.

Kabla ya kusaini mkataba mpya, mkataba wa awali wa Firmino mwenye umri wa miaka 26, ulitarajiwa kufikia kikomo mwishoni mwa msimu 2019-20.

Mkataba mpya aliousaini utamuwezesha Firmino ambaye tayari ameshaitumikia timu yake ya taifa katika michezo 19 na kufunga mabao 5, kukaa klabuni hapo hadi mwaka 2023 na atalipwa mshahara wa Pauni laki moja na elfu themanini (180,000), kwa juma.

Firmino amekua na uhusiano mzuri katika safu ya ushambuliaji ya Liverpool dhidi ya washambuliaji wengine klabuni hapo Sadio Mane na Mohamed Salah, ambao pia wanategemewa kusaini mikataba mipya siku za usoni.

Arjen Robben kuikosa Real Madrid kesho
Zinedine Zidane: Tutashambulia mwanzo mwisho