Aliyekua meneja wa klabu ya Everton Roberto Martinez ametangazwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ubelgiji.

Martinez ametangazwa kuchukua nafasi hiyo, baada ya chama cha soka nchini Ublegiji kumtimua Marc Wilmots siku chache baada ya kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kuondolewa katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Euro 2016 kwa kufungwa na Wales mabao matatu kwa moja.

Uteuzi wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 43, umepokelewa kwa mshangao mkubwa na mashabiki wengi wa soka, kutokana na ukimya uliokua umetawala baina ya viongozi wa chama cha soka nchini Ubelgiji dhidi ya Martinez.

Martinez, ambaye ni raia wa nchini Hispania, alifukuzwa Goodison Park mwezi Mei mwaka huu, baada ya kushindwa kufikia malengo yaliyokua yamekusudiwa na viongozi wa klabu ya Everton ambayo aliitumikia kwa muda wa miaka mitatu.

Klabu nyingine ambazo Martinez ameshazitumikia akiwa nchini England ni Swansea City na Wigan Athletic ambayo aliiongoza kutwaa ubingwa wa kombe la FA mwaka 2013.

Man City Wafanya Kweli Kwa Kinda La Kibrazil
Video: NEMC imetangazafaini wananchi wanaokaa karibu na mifereji