Meneja wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers amekiri kushangazwa na maamuzi yaliyochukuliwa na kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Carlos Dunga ya kumtema kiungo mshambuliaji Philippe Coutinho Correia.

Rodgers, amesema haimuingii akilini kuachwa kwa kiungo huyo ambaye kwa sasa ameonyesha kiwango kikubwa akiwa na kikosi cha Liverpool kilichoanza vyema mshike mshike wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Amesema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, nae ameshangazwa na maamuzi hayo, kutokana na kufahamu wazi huenda angekua sehemu ya kikosi kilichoitwa na kocha Dunga tayari kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Costa Rica utakaochezwa Septemba 5.

Coutinho kwa mara ya mwisho aliitwa kwenye kikosi cha Brazil wakati wa fainali za mataifa uya Amerika ya kusini (Copa America) zilizofanyika nchini Chile miezi miwiwli iliyopita.

Kuuachwa kwa kiungo huyo aliyeifungia bao pakee Liverpool kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi ya nchini England msimu huu dhidi ya Stoke City, kumetoa nafasi ya kuitwa kwa kiungo wa klabu ya Orlando City ya nchini Marekani, Ricardo Kaka.

Kikosi kamili cha Brazil kilichoitwa kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Costa Rica.

Makipa: Jefferson (Botafogo), Marcelo Grohe (Grêmio), Alisson (Internacional)

Mabeki: Daniel Alves (Barcelona), Danilo (Real Madrid), Filipe Luís (Atlético Madrid), Douglas Santos (Atlético-MG), Miranda (Internazionale), David Luiz (PSG), Gabriel Paulista (Arsenal), Marquinhos (PSG)

Viungo: Luiz Gustavo (Wolfsburg), Elias (Corinthians), Ramires (Chelsea), Fernandinho (Manchester City), Oscar (Chelsea), Douglas Costa (Bayern Munich), Willian (Chelsea)
Lucas Lima (Santos), Kaká (Orlando City)

Washambuliaji: Neymar (Barcelona), Roberto Firmino (Liverpool), Lucas (PSG), Hulk (Zenit)

Stars Kumkosa Mshambuliaji Wa Mansfield Town
Waamuzi Wa Ligi Kuu Kupigwa Msasa