Mcheza tenesi raia wa Switzerland Roger Federer ameweka rekodi mya baada ya kuwa mchezaji wa kwanza kushinda taji la michuano ya Wimbledon kwa mara ya nane.

Federer ambaye ni mchezaji namba tano kwa ubora wa chezo wa tenesi duniani ametwaa taji hilo baada ya kumshinda Marin Cilic kwa jumla ya seti tatu.

Katika seti ya kwanza Federer alishinda kwa  6-3 kisha akashinda kwa 6-1 na kumaliza kwa 6-4, katika mchezo uliochezwa kwa muda wa saa moja na na dakika 41.

Hili ni taji la 19 la Grand Slam kwa bingwa huyu wa kihistoria mwenye miaka 35  na kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kutwaa mataji yote ya michuano ya wazi ya England.

”Kubeba kombe bila kupoteza seti hata moja katka mashindano ni jambo la kushangaza nasindwa kuamini nia furaha sana” aliseama Roger Federer.

 

Raila afunguka kama atakubali matokeo akitangazwa kushindwa
Auawa akisubiri kupiga kura ya maoni

Comments

comments