Siku chache baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kutoa tamko la kuufungia wimbo wa Roma ‘Viva’, rapa huyo amesema kuwa bado hajapata barua rasmi ya Baraza hilo.

Amesema yeye pia ameiona habari hiyo kwenye akaunti ya Instagram ya chombo kimoja cha habari na sababu zilizoainishwa na Baraza hilo kuifungia ‘Viva’.

Licha ya kukiri kuwa hafahamu taratibu zinazotumiwa na Baraza hilo kutoa taarifa kama hizo, Roma alilishauri Baraza hilo kuweka utaratibu wa kuzisikiliza nyimbo kabla hazijatoka ili kuepusha usumbufu.

“Nisiwe muongo sijui taratibu kinakuwa kinatumia kufikisha information zao, kwa sababu kitu ambacho naona ingekuwa rahisi kama artist kabla hajaachia nyimbo yake mpya ama hajafanya kazi yake ya sanaa, iwe inawasilishwa katika hiko chombo, nadhani hapo tungekuwa tunaenda sawa,” alisema. Roma.

Hata hivyo, Afisa Habari wa Basata, Artistide Kwizela alifafanua taratibu zinazotumiwa na Baraza hilo kufikisha ujumbe wake kwa umma pale wanapofungia kazi ya msanii fulani.

“Kuna kufungia kwa maana ya msanii mwenyewe kuandikiwa, lakini kama kuna taarifa imetoka public kwamba nyimbo za namna hiyo zimezuiliwa, kuna two way either barua kuandikwa kwa msanii au pia kuna public anouncements kwamba wimbo fulani umefungiwa.”

Mourinho Awashangaza Waandishi Wa Habari
CCM Yamtimua Mwandishi Wa Mwananchi Kwenye Timu Ya Wana Habari, Kisa…