Roma Mkatoliki ameamua kufunga mdomo wake na kuachana na tukio la kutekwa nyara ili kunusuru maisha ya muziki wake.

Rapa huyo kutoka Tanga amefunguka kupitia Friday Night Live ya East Africa TV kuwa baada ya kutafakari alibaini kuwa kama angeeleza ukweli wote wa tukio la kutekwa akiwa na wenzake wawili ndani ya studio za Tongwe Records ingeweza kuwa mwisho wa muziki wake na mwanzo wa safari ya kurejea nyumbani kwao kushiriki shughuli za kilimo.

“Pengine hiyo story ambayo watu wangetaka waisikie ingesemwa, pengine ndio ingekuwa mwisho wa Roma kwenye career yake ya muziki. labda mashabiki wangeshangilia lakini [makampuni yote ya simu] biashara yao na Roma ndio ingeishia hapo,” Roma amefunguka.

“Kwahiyo, mwisho Roma angerudi Tanga ashike jembe aanze kulima. Je, mashabiki hilo wangependa? Kwanini Roma asiendelee kubaki halafu akatoa nyimbo zake dude baada ya dude?” Alihoji.

Mkali huyo wa michano alisisitiza kuwa anajipanga kuachia wimbo wake mpya wakati wowote. Alisema kuwa tamasha alilofanya hivi karibuni katika ukumbi wa Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam limempa moyo na kuona jinsi ambavyo mashabiki wako tayari kumpokea tena.

Roma na wenzake wawili akiwemo rapa Moni walitekwa na watu wasiojulikana wakiwa ndani ya studio za Tongwe Records na kuachiwa baada ya siku tatu wakiwa na majeraha makubwa yaliyotokana na mateso wayoyopata.

Chin Bees amvimbia Chid Benz, ‘mimi nafanya yangu’
Picha: Mwili wa Shaban Dede wazikwa jijini Dar es salaam