Kaka wa mwanamuziki Diamond Platnumz ambaye pia ndio Dj wake maalum, Romy Jones amemuandikia barua ya wazi mwanamuziki huyo ikiwa na ujumbe mzito kuhusu matukio anayodai kuwa ni ya kusalitiwa, kutukanwa na hata kuonekana hana thamani baada ya kuwasaidia baadhi ya wasanii waliosainiwa na WCB Wasafi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Romy amebainisha kuwa kuna mambo kadhaa mabaya  yanayoendelea, yenye kumuhusu Diamond na wasanii aliowahi kuwasaini kwenye rekodi label yake.

ISEMAVYO BARUA YA ROMMY KWA DIAMOND.

“Barua ya wazi kwa mdogo wangu Nassib Abdul ama Diamond Platnumz, nakumbuka ulivyoanza kutoa nyimbo na wasanii tofauti, soko lako hadi namba zako zilianza kukua kwa kasi sana kwenye muziki wako hadi kupelekea kuwa msanii bora wa Afrika Mashariki,”.

Sio sababu wewe ndio ulikuwa unajua kuimba peke yako, Hapana, bali ulikubali kuwekeza muda, akili hadi pesa kwenye biashara yako hadi ikafika kipindi tukawa tunashangaa kolabo zako.

Mara na Davido, Psquare mara Mr Flavour na ndio watu waliokuwa moto kweli kweli kipindi hicho.

Ushauri wa wazi kwako, hata kama ni biashara au kukuza vipaji vya mtaani nadhani inatosha, kwanini usiwekeze nguvu, Akili na pesa kwenye biashara yako ya Radio na Tv?.

Wanasema kikulacho kinguoni mwako, wale wale uliowafungulia njia ndio wapo nyuma yako kukukashifu, kukuponda hata kukukebehi.

Tukiangalia Top charts za wasanii wote ni wale waliotoka kwako ama waliopo kwako, hii ni wazi kwamba usingekuwa na wasanii namba za mwanzo zote huenda zingekuwa za kwako kwa kipindi kirefu mno.

Ni kweli kila anayekuwa anahitaji kutoka kwenye familia na kujitafutia ugali wake mwenyewe na kutengeneza familia yake, sasa ni lazima kumponda na kumkebehi mzazi wako??

Lil wayne bado yupo na wakina Drake na juzi walitumbuiza pamoja kwente tamasha la Drake, Usher Raymond bado yupo na Justine Bieber na anaendeleq kunufaika na matunda yake, sijajua huku kwetu ni ulimbukeni wa pesa nyingi za ghafla, tabia au uelewa ni mdogo!.

Jaribu kuwekeza nguvu zako kwako mwenyewe tuone, kwa sasa hivi huenda ungrkuwa na album moja na Chris Brown, kuliko kuwekeza nguvu na muda kwa watu wasio na shukurani, naomba kuwasilisha” AMEHITIMISHA ROMMY.

Punde baada ya ujumbe huo mzito wa Romy Jones, Mwanamuziki Diamond Platnumz amemjibu kaka yake kufuatia suala hilo.

MAJIBU YA DIAMOND KWA ROMMY.

“Hivi saa ndio nimegundua kwanini watu kama kina Kidayo, davido na kadharika waliamua kufocus na nafsi zao na sio kupoteza nguvu, umaarufu, pesa na muda wao kusaidia wasanii chipukizi walio wasign, hii industry haina shukran, but usiumie hii ni nchi yetu na ni jukumu letu kuhakikisha kwamba tunaendelea
kunyanyua vijana toka mtaani ili nao wajikomboe kimaisha.” AMEMALIZA DIAMOND.

Barua hiyo, na majibu ya wazi kutoka kwa Romy Jones na Diamond inakuja muda mfupi baada ya msanii Rayvanny kujiengua chini ya usimamizi wa Diamond na kuvhukua uamuzi wa kujitegemea, wakati ambao takribani miaka miwili msanii Harmonize naye alijitoa chini ya uongozi huo jambo lililoibua gumzo kubwa.

Rais wa FIFA, CAF kuitazama Kariakoo Derby Jumamosi
Kenya: Wapiga kura milioni 10 wasusia uchaguzi