Mshambuliaji kutoka nchini Ureno, Crisitiano Ronaldo amefichua siri iliyodumu kwa zaidi ya miaka mitano tangu alipoondoka Man Utd na kujiunga na Real Madrid mwaka 2009.

Ronaldo amesema alikuwa haongei na Rio Ferdinand, Ryan Giggs na Paul Scholes akiwa nje ya uwanja, lakini suala hilo lilikua halifahamiki kutokana na umoja uliokua umeimarishwa kwenye kikosi na meneja wa Man Utd kwa wakati huo Sir Alex Ferguson.

Mshambuliaji huyo alifichua jambo hilo baada ya kuulizwa kuhusu uhusiano wake na wachezaji wenzake katika safu ya ushambuliaji ya Real Madrid, Karim Benzema na Gareth Bale, ambao unaonekana kuwa mbovu kulinganisha ilivyo kwa washambuliaji wa FC Barcelona, Luis Suarez, Lionel Messi na Neymar.

Ronaldo amesema mahusiano dimbani hayana maana yoyote, na kwamba kilicho muhimu ni kupigana kwa ajili ya kutafuta maslahi bora ya klabu.

“Nitakueleza kitu,” alisema Ronaldo katika mkutano na waandishi wa habari Jumanne.

“Wakati nilipokuwa United, sikuwa nazungumza (nje ya uwanja) na Giggs, Scholes na Ferdinand mbali ya salamu ya kawaida ‘habari ya asubuhi’, lakini tulishinda Champions League (2008).

“Tulizungumza uwanjani na hilo ndilo lilikuwa muhimu kwa wote. Je, ni jambo muhimu kwamba siendi kwenye chakula cha jioni na Benzema au kwamba Bale haji nyumbani kwangu? Si muhimu.

Hili jambo kuhusu milo kidogo, makumbatio madogo, mabusu kidogo kwangu halina maana yoyote,” alisema.

Uchaguzi Uganda: Museveni aeleza sababu za kuzima data, mawasiliano na huduma za kifedha
Juventus Yatangaza Vita Kali Dhidi Ya Arsenal, Man Utd