Mshambuliaji wa mabingwa wa Soka Italia Juventus FC, Cristiano Ronaldo ameandika historia kwa mara nyingine katika mchezo wa Ligi Kuu Italia ‘Serie A’ dhidi ya SSC Lazio ya kuwa mchezaji wa kwanza kupachia mabao 50 kwenye ligi tatu tofauti.

Bao alilofunga na Mreno huyo kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati dhidi ya SSC Lazio, lilimfanya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi ndani ya nusu karne (miaka 50) tangu ajiunge na miamba hiyo ya soka la Italia.

Amekuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi ndani ya muda mfupi tangu mwaka 1995. Kwa kuongezea, mshambuliaji huyo mwenye miaka 35, bao lake hilo alilofunga kipindi cha pili, limemfanya pia kuwa sawa na Giuseppe Signori ambaye ndani ya msimu mmoja (1994-95) alipachika mabao 12 kwa njia ya penati.

Habilidades PES e FIFA: Habilidades Giuseppe Signori
Giuseppe Signori

Ronaldo alijiunga na Juventus FC wakati wa msimu wa 2018/19 baada ya kufanya vizuri akiwa na miamba ya soka la Hispania, Real Madrid ndani ya miaka 10, ambapo alitwaa mataji mbalimbali ikiwemo manne ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Kabla ya hapo, aliichezea kwa miaka sita Manchester United, ambako alitwaa tuzo yake ya Ballon d’Or  mwaka 2008 baada ya kufanya vizuri akiwa na kikosi hicho cha mashetani wekundu wa Old Trafford.

Katika klabu zote ambazo amezichezea amekuwa na urafiki mzuri na nyavu, alipachika mabao 118 katika michezo 292 aliyoichezea Manchester United, mabao 450 kwenye michezo 438 akiwa na Real Madrid na sasa akiwa na ‘kibibi kizee cha Turin’ ameendelea kuuwasha moto.

Upande wa  kimataifa akiwa na timu yake ya Taifa la Ureno, Ronaldo amepachika mabao 99 katika mashindano yote, amezidiwa mabao 10 tu na kinara wa mabao wa muda wote katika ngazi hiyo, Ali Daei ambaye ni raia wa Iran akiwa na mabao 109.

Juventus FC  ambao wapo katika vita ya kuwania ubingwa wa  Serie A kufuatia ushindi ambao waliupata jana wa mabao 2-1 dhidi ya Lazio yote yalifungwa na Ronaldo, wamefikisha alama 80 kwenye kilele cha msimamo wa ligi hiyo huku wakifuatiwa na Inter Milan wenye alama 70.

Waziri Mkuu atoa wito Watanzania mipakani kulinda nchi
CCM Kawe wamkataa Gwajima Ubunge 2020