Mchezaji wa Klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo jana aliisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa Vilabu bingwa barani Ulaya huku akiweka rekodi nyingine ya ufungaji bora katika mashindano hayo.

Katika mchezo wa fainali uliofanyika jana katika uwanja wa Cardiff nchini Wales, Ronaldo aliipachikia magoli mawili timu yake huku mengine yakitiwa kambani na wachezaji wenzie kukamilisha ushindi wa goli 4-1 dhidi ya Juventus.

Mabao hayo mawili yamemfanya amzidi mshindani wake mkuu katika soka, Lionel Messi wa Barcelona ambaye alikuwa na mabao 11 hivyo kuweka rekodi mpya katika mashindano hayo makubwa barani ulaya

 

Trump, Macron, Mirkel walaani shambulio la kigaidi nchini Uingereza
Uteuzi wa IGP Sirro wazua shangwe mkoa wa Pwani