Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Christiano Ronaldo amependekeza klabu hiyo kumsajili kiungo mshambuliaji wa Paris Seint Germany (PSG) ya Ufaransa, Goncalo Guedes ili kuchukua nafasi ya  Gareth Bale katika usajili wa msimu wa joto.

Kwa mujibu wa mtandao wa Diario Gol, Ronaldo amempendekeza mchezaji huyo kinda (21) kufuatia kuonesha uwezo mkubwa katika msimu huu kwenye ligi kuu nchini hispania akiichezea klabu ya Valencia kwa mkopo kutoka PSG.

Hata hvyo, Raisi wa klabu hiyo Florentino Perez ameonesha kupingana na mapendekezo yaliyotolewa na Ronaldo baada ya kusemekana amedhamilia kumsajiri Neymar kuchukua nafasi hiyo.

Bale ameingia kwenye orodha ya wachezaji wenye majina makubwa ndani ya real Madrid ambao wanatarajiwa kuondoka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu, na tayari timu kubwa nchini Uingereza zikiwemo Chelsea,Tottenham na Mancherster United zimeshaonesha lengo la kumsajili

Joachim Low: Tunaiheshumu Brazil
Marekani yawafukuza Wanadiplomasia 60 wa Urusi

Comments

comments