Wakati dunia na ulimwengu wa soka kwa sasa unaomboleza msiba wa msafara wa timu ya Chapocoense ya Brazil uliopata ajali wakati wakielekea kutua uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Medellin nchini Colombia, mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametoa mkono wa pole wa kitika cha fedha.

Ajali hiyo ya ndege iliyotokea jana iliwahusisha watu 81, kati ya hao 76 wamepoteza maisha huku 72 kati yao walikuwa ni sehemu ya msafara wa timu hiyo na wachezaji wakielekea kucheza mchezo wao wa fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Amerika kusini dhidi ya Atletico Nacional ya Colombia.

Cristiano Ronaldo ni mmoja kati ya mastaa wa soka walioguswa kwa kiasi kikubwa na msiba huu na ameamua kuchangia euro milioni 3 ambazo ni zaidi ya Shilingi za Tanzania bilioni 9.6 kwa timu ya Chipacoense na familia za wachezaji wa timu hiyo waliyopoteza maisha.

Chadema: Hatutakubali tena kudhulumiwa 2020
Juventus Yajishtukia Kwa Paulo Dybala