Mwaka 2016 umekuwa mwaka wa Cristiano Ronaldo, sio tu kwenye ulimwengu wa soka, hata nje kwenye mitandao ya kijamii.

Mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or wa mwaka huu, ambaye pia ana sababu nyingi za kuuita mwaka huu ‘mwaka wa neema’ kwa kushuhudia timu yake ya Real Madrid ikitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na timu yake ya taifa ya Ureno ikibeba kombe la Mataifa ya Ulaya, ametajwa kuiteka pia mitandao ya kijamii.

Taarifa za kiuchambuzi kutoka kwa taasisi ya uchambuzi wa mitandao ya kijamii ya CrwodTangle imemtaja Ronaldo kuwa mfalme wa mitandao ya kijamii kati ya wanamichezo wote duniani akiweka rekodi ya post tatu zilizopendwa zaidi duniani kwenye mtandao wa Facebook, na posts tano zilizopata nafasi za juu zaidi kwenye Instagram.

Posts zake kwa ujumla wake zilivuta jumla ya watu milioni 34 waliozijadili kwa namna mbalimbali.

Picha za Ronaldo zilizoongoza kwenye Facebook mwaka huu ni pamoja na ile inayomuonesha akiwa amebeba kombe la Ulaya, nyingine ni ile inayomuonesha akisherehekea siku yake ya kuzaliwa pamoja na ile inayomuonesha akiwa ndani ya ndege nakikosi cha Ureno. Post iliyoongoza Facebook iliwavuta watu zaidi ya milioni 7.4

 

Tanzia: Mwimbaji Mkongwe George Michael afariki akirekodi filamu
Hupaswi kukosa jibu hili la Lowassa kuhusu hatma ya urafiki wake na Kikwete