Mshambuliaji hatari wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametangaza msimamo wa kutokua tayari kuiacha klabu hiyo ya mjini Madrid katika kipindi hiki, ambapo bado mkataba wake unaendelea kufanya kazi hadi mwaka 2018.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 31, amelazimika kuweka bayana mpango huo, baada ya kuhusishwa kwa muda mrefu na taarifa za kutaka kurejea kwenye klabu ya Man utd ama kujiunga na mabingwa wa nchini Ufaransa PSG.

“Nataka kubaki hapa kwa miaka miwili zaidi, miaka miwili ninayoizungumzia itanichukua hadi mwisho wa mkataba wangu,” alinukuliwa mchezaji huyo akisema.

“Hii ni Ligi bora duniani, japokuwa pia nimecheza Ligi ya England, ni Ligi ya ushindani na ina wachezaji wazuri,” aliongeza staa huyo.
Ronaldo alizungumza hayo wakati wa hafla ya uchukuaji tuzo ya Pichichi, ambayo hutolewa kwa mfungaji bora nchini Hispania.

Ronaldo alifanikiwa kufunga mabao 48 katika ligi ya nchini Hispania msimu wa 2014-15.

Vibosile Wa Liverpool Wafunga Breki Kwa Mashabiki
Angalia Orodha Ya Klabu 10 Bora Barani Afrika