Gwiji wa soka nchini Brazil ambaye amewahi kushinda Kombe la Dunia Ronaldo de Lima amesikitishwa sana kitendo cha Lionel Messi kustaafu soka la kimataifa, lakini bado akiwa na matumaini kwamba atafuta maamuzi yake na kurejea tena kwenye medani hiyo.

Mshambulizi huyo wa Barcelona (29), akiwa na Argentina Jumapili iliyopita alipoteza fainali yake ya tatu ndani ya miaka mitatu katika michuano mikubwa ngazi ya timu ya taifa  na kushuhudia Chile wakibeba ndoo ya Copa America kwa mara ya ili mfululizo mikononi mwao kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Messi, akiwa amekosa mkwaju wa penati, aliushangaza na kuushtua ulimwengu baada ya tukio lile kufuatia kutangaza kutochezea tena Argentina, na kusababisha maelfu ya watu akiwemo Diego Maradona na rais wa nchi hiyo kutoka hadharani na kumsihi kufikiria upya juu ya maamuzi yake.

Ronaldo, ambaye pia alikumbana na hali kama hiyo ya kupoteza michezo katika fainali za Kombe la Dunia na Copa America kabla ya kufanikiwa kushinda yote kwa pamoja, kama ilivyo kwa mamilioni ya wapenda soka ulimwenguni amemsihi Messi kubadilisha uamuzi wake na kurejea katika timu ya taifa.

“Ni kweli hayo ni maamuzi binafsi zaidi kwa Messi na sisi sote tunaheshimu,” Ronaldo aliliambia Shirika la habari la China la Xinhua.

“Sote tunajisikia vibaya kwa maamuzi ya Messi na tunaamini atabadili mawazo yake.”

Watu Sita Wamefariki Katika Shambulio Kenya
Joseph Marius Omog Asaini Miaka Miwili Simba