Gwiji wa soka duniani Ronaldo Luís Nazário de Lima, amezungumzia ubora wa wachezaji wanaotikisa dunia kwa sasa Cristiano Ronaldo wa Real Madrid  pamoja na Lionel Messi wa FC Barcelona.

Ronaldo ambaye alicheza soka kwa mafanikio makubwa kati ya mwaka 1994 hadi 2014, amesema wachezaji hao wawili wote wana viwango bora, lakini katika kipindi hiki anaamini wa jina lake ana uwezo zaidi kuliko Lionel Messi.

Amesema mara kadhaa amekua akifuatilia ubishani unaendelea katika mitandao ya kijamii pamoja na mijadala mbali mbali kupitia vyombo vya habari kuhusu wawili hao, lakini amepima na kuona Ronaldo ana uwezo zaidi.

Hata hivyo Ronaldo De Lima ameutaka umma wa wapenda soka kutomuelewa vibaya kuhusu mawazo yake, kwani kabla ya kujitokeza hadharani alikua akiamini na kuheshimu michango ya wengine kuhusu wachezaji hao.

Katika hatua nyingine Ronaldo amefafanua kwa nini ameona Cristiano ni bora katika kipindi hiki, kwa kusema mchezaji huyo amekua muhimili mkubwa wa kuisaidia klabu yake ya Real Madrid hususan msimu uliopita pamoja na timu yake ya taifa ya Ureno.

Cristiano alikua sehemu ya kikosi cha Real Madrid ambacho kilitwaa ubingwa wa ligi ya barani Ulaya, na majuma kadhaa baadae aliongeza chachu ya ushindi kwa taifa lake kupitia michuano ya Euro 2016 iliyofanyika nchini Ufaransa.

Kwa upande wa Lionel Messi, Ronaldo De Lima amesema hakua na msimu mzuri na alishindwa kuisaidia timu yake ya taifa ya Argentina katika fainali za mataifa ya kusini mwa Amerika (Copa America), hivyo haamini kama mshambuliaji huyo ana kigezo cha kuitwa mbora kwa wakati huu.

Mtazamo huo wa Ronado De Lima umekuja huku wachezaji hao wawili wakiwa sehemu ya wanaowania tuzo ya mchezaji bora duniani, ambayo hutolewa kila mwaka na shirikisho la soka ulimwenguni FIFA.

Ziara ya Makamba yatua Maabara ya Chura wa Kihansi, azuru misitu na vijiji Iringa
Waharibifu wa mazingira wakamatwe - Waziri Mkuu