Mshambuliaji kutoka nchini Ureno, Cristiano Ronaldo yupo hatarini kufungiwa michezo minne hadi 12, kutokana na kitendo cha kumsukuma mwamuzi wakati wa mchezo wa Supercopa de Espana, uliofanyika usiku wa kuamkia leo nchini Hispania.

Ronaldo ambaye alifunga bao moja katika mchezo huo uliowakutanisha dhidi ya FC Barcelona, alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kujiangusha eneo la hatari la wapinzani, na ndipo mwamuzi akampa kadi ya pili ya njano lakini wakati akilalamika, alimsukuma mgongoni.

Hata hivyo mamuzi ya kuongezewa adhabu kwa mshambuliaji huyo, kunategemea na maazimio ya kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka nchini Hispania, ambayo itapitia ripoti iliyowasilishwa na mwamuzi huyo.

Kwa mujibu wa kifungu cha 96 cha kanuni za soka za Chama cha Soka cha Hispania kitendo cha kumsukuma mwamuzi kinaweza kumfanya mchezaji afungiwe mechi nne hadi 12.

Endapo Ronaldo atakumbana na adhabu ya kufungiwa michezo minne hadi 12, atakosa sehemu ya kwanza ya msimu wa ligi ya Hispania ambayo itaanza mwishoni mwa juma hili.

Maporomoko ya ardhi yaua mamia Sierra Leone
Habari picha za Rais wa Misri alivyowasili nchini mapema hii leo