Polisi wa Las Vegas nchini Marekani wametoa wito rasmi wa kutaka sampuli ya vinasaba (DNA) vya mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa tuhuma za ubakaji.

Mchezaji huyo Mreno mwenye umri wa miaka 33, anatuhumiwa kumbaka Kathryn Mayorga katika hoteli moja ya kifahari iliyoko Las Vegas mwaka 2009.

Jarida la The Wall Street limeeleza kuwa wito huo wa polisi umetumwa kwenye mfumo wa Mahakama nchini Italia ili Ronaldo aelekezwe kuwasilisha sampuli hizo.

Mwanasheria wa Ronaldo, Peter S. Christiansen ameviambia vyombo vya habari kuwa wito huo ulikuwa wa kiuweledi na kwamba sio kitu kinachowashangaza kutokana na tuhuma zilizokuwepo.

“Ronaldo anaendelea kuwaeleza kama anavyofanya leo [kuwa tuhuma hizo sio za kweli]. Kwahiyo haishangazi kuwa polisi wanaomba sampuli za DNA kiuweledi kama sehemu ya uchunguzi wao,” imeeleza taarifa iliyoandikwa na Christiansen.

Jarida la Ujerumani linalotoka kila wiki la Der Spiegel, ambalo lilikuwa la kwanza kuchapisha tuhuma hizo Oktoba mwaka jana, limeeleza kuwa Mayorga aliwasilisha malalamiko yake polisi, Las Vegas.

Cristiano Ronaldo na Kathryn Mayorga wakiwa kwenye starehe mwaka 2009

Jarida hilo lilieleza kuwa mwaka 2010, Ronaldo na Mayorga waliingia makubaliano ya kuyamaliza nje ya mahakama na kusaini makubaliano ya kutoweka hadharani kilichotokea ambapo alilipwa $375,000.

Mwanasheria wa Ronaldo ameeleza kuwa mteja wake hakatai kuwa alisaini makubaliano na Mayorga, lakini hiyo haimaanishi kuwa makubaliano hayo ni kukiri kuwa na hatia.

Moto wa Ali Kiba, Diamond, Chris Brown wawatibua Wakenya, wawaponza wanasiasa
Wanaodaiwa kumuibia Mugabe begi lililojaa pesa waisoma namba