Mchezaji wa zamani wa Brazil, Pele ametoa mawazo yake kuhusu nafasi ya nahodha wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar kuwa mchezaji bora wa dunia.

Akizungumza na Gazzeta World, Pele alisema kuwa anaamini Neymar ana uwezo lakini atakuwa mchezaji bora wa dunia baada ya miaka kadhaa kutokana na kuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Messi na Ronaldo.

“Kwa sasa mchezaji bora wa dunia ni Messi, na pia hata Ronaldo ni mchezaji mzuri lakini kwa kipindi cha miaka miwili ijayo naamini Neymar atakuwa mchezaji bora wa dunia, alisema Pele.

Arsenal Walazimisha Mazungumzo Ya Usajili Wa Granit Xhaka
Haji Manara Apata Ajali Ya Barabarani