Mbabe Ronda Rousey amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu kipigo alichopokea kutoka kwa Amanda Nunes katika pambano lao la UFC 207 Disemba 2016.

Ronda amekuwa akikataa kuzungumzia pambano hilo lililomlazimisha kustaafu mapambano hayo kikiwa ni kipigo cha pili kilichoweka doa kwenye rekodi yake ya kutopigika, lakini wikendi hii aliamua kuzungumza huku machozi yakitembelea macho yake.

“Ninakumbuka pambano hilo la kwanza, nilitembea huku nafikiria, ‘Mungu ananichukia’. Sikuwa na kitu kilichobaki,” alisema.

“Lakini sio kitu kibaya ambacho natakiwa kukionea aibu. Ni kitu ambacho natakiwa nikipokee na niendelee kuionesha dunia kuwa mimi ni bora, na ndiyo sababu niko hapa,” aliongeza Ronda ambaye hivi sasa anashiriki mapambano ya mieleka (WWE).

Alisema kuwa mumewe amekuwa akimshika mkono katika hali zote na kumpa moyo wa kuendelea kushiriki mapambano.

‘Aliyefungia nyimbo za wasanii sio Shonza’
JPM amtumbua Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi NHC, avunja bodi ya shirika hilo