Mshambuliaji na nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney amesema kuwa ni heshima kubwa kwake kuifikia rekodi nzito ya magoli iliyokuwa ikishikiliwa na Sir Bobby Charlton  na kwamba ana kiu ya kuivunja.

Rooney mwenye umri wa miaka 31 aliifikia rekodi ya Charlton jana baada ya kufunga goli moja kati ya manne katika dakika ya 6 ya mchezo dhidi ya Reading, na kumfanya kufikisha magoli 249 ndani ya klabu hiyo kwa mechi 537, sawa na magoli yaliyofungwa na Charlton ambaye sasa ni gwiji na mkongwe mwenye umri wa miaka 79, kwa mechi 758.

“Ni wakati wa kujivunia. Tuna michezo mingine miwili ya nyumbani kwahiyo natumaini nitapata goli moja la ziada kati ya michezo hiyo,” alisema Rooney.

United itakutana na Hull City Jumanne ijayo katika nusu fainali ya EFL kabla ya kukutana na kisiki cha Liverpool Januari 15 kwa mchezo wa Ligi Kuu.

Akizungumzia hatua hiyo, Kocha Jose Mourinho alieleza kufurahishwa huku akisisitiza kuwa siku nzuri zaidi kwa Rooney inakuja hivyo anahitaji goli moja la ziada kuifunika rekodi hiyo na kuwa kileleni peke yake.

“Ilikuwa nzuri sana lakini ninahitaji goli moja la ziada. Ni mtu mzuri sana kwenye kikosi na sisi tunataka afanye hivyo. Kuwa na Wayne kama mchezaji anayeshikilia rekodi ya kufunga magoli mengi zaidi kwenye timu hii ni nzuri sana kwake,” alisema Mourinho.

Mchezaji wa zamani wa Manchester Utd, Jaap Stam pia ni mmoja kati ya waliompa mkono wa kheri Rooney kwa hatua aliyoipiga. Alisema anafurahia hatua hiyo kwakuwa Rooney alikuwa mchezaji mzuri tangu mwanzo.

Lowassa atoa neno kwa waliomtabiria kifo
Millard Ayo aanza kazi ‘Citizen TV’ ya Kenya