Aliyekuwa mshambuliaji wa timu ya Taifa ya England, Wayne Rooney amewasili rasmi katika klabu yake mpya ya DC United inayoshiriki Ligi Kuu Marekani MLS.

Rooney amewasili DC United Juni 28, 2018 akitokea Everton ya England na kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu na ataanza kutambulika kama mchezaji  rasmi wa DC United, dirusha la usajili litakapofunguliwa July 10 2018.

Rooney ambaye amewahi kuwa nahodha wa Man United na timu ya taifa ya England, amewasili Airport na kupokelewa na mamia ya mashabiki ambao wamefurahishwa na ujio wake katika club yao.

 

 

Video: Ni mshikemshike bungeni Dodoma, Mvutano mkali kesi ya kina Mbowe
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 29, 2018

Comments

comments