Nahodha na mshambuliaji wa klabu ya Man Utd, Wayne Rooney amejihukumu yeye mwenyewe, kwa kusema hadhani kama ataendelea kuitumikia timu ya taifa ya England ndani ya miaka miwili ijayo.

Rooney ametangaza matarajio hayo, ikiwa ni siku kadhaa zimepita baada ya chama cha soka nchini England FA, kumthibitisha Sam Allardyce kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo (The Three Lion).

Mshambuliaji huyo amesema hata kama itatokea, anathibitishia nafasi ya kuendelea kuwa nahodha kwenye kikosi cha timu ya taifa, bado anaamini hana muda mrefu wa kuendelea kuitumikia The Three Lion.

Hata hivyo mpaka sasa, Sam Allardyce bado hajazungumza jambo lolote kuhusu nani atakuwa nahodha wa kikosi chake, ambacho mwanzoni mwa mwezi ujao kitaanza kampeni ya kusaka tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2018.

Alipokutana na waandishi wa habari katika mkutano maalum wa kutambulishwa kwake, Allardyce alisema, maamuzi ya nani atakua nahodha wa kikosi cha The Three Lion yatapatikana mara baada ya kukutana na wachezaji atakaowaita kikosini mwezi huu.

England itaanza kampeni ya kusaka tikeki ya kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, kwa kupambana na Slovakia.

Mnangagwa akanusha madai kupindua Serikali ya Mugabe
Schalke 04 Wakanusha Taarifa Za Leroy Sane