Mfanyabiasha maarufu nchini, Rostam Aziz amemtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam kwa ajili ya kumpongeza kwa kazi nzuri anayoifanya.

Amesema kuwa kwasasa rais Magufuli anatengeneza misingi ya usawa katika biashara ili kila mmoja apate anachostahili na si vinginevyo.

Aidha, ameongeza kuwa kinachofanyika hivi sasa ni kuwawezesha watu kufanyabiashara zao kwa uhuru na haki tofauti na hapo awali.

“Nimekuja kumuona na kumpongeza mwenyekiti wangu wa chama na rais wangu kwa kazi nzuri anayoifanya, anacho kifanya kwasasa ni kuweka usawa katika biashara, watu wawe huru,”amesema Rostam

Hata hivyo, ameongeza kuwa mazingira anayoyatengeneza rais Magufuli yatasaidia kuweza kuinua uchumi kwa haraka zaidi.

Rayvany afunguka kuhusu wimbo wake wa Mwanza
Nchi hii imejaa hofu kila kona- Godbless Lema

Comments

comments