Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson amewataka wachezaji wanaounda kikosi chake, kufanya kila linalowezekana ili wafanikishe mpango wa kutwaa ubingwa wa barani Ulaya (Euro 2016), kama ilivyo kwa mabingwa wa soka nchini humo Leicester City.

Hodgson ametoa wito huo, siku moja baada ya kutaja kikosi chake cha wachezaji 26, ambacho kitaingia kambini kujiandaa na fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016 (Euro 2016), zitakazoanza rasmi juni 10 nchini Ufaransa.

Kocha huyo amesema anaamini hakuna litakaloshindana kufikia malengo hayo, endapo wachezaji wake watajituma wakati wote na kuelekeza akili zao katika mkakati wa kupambana kila watakapokua wakiingia uwanjani na kuzitumikia vyema dakika 90.

Amesema siri ya kusaka mafanikio ni kujitambua na kuliweka dhamira jambo ulitakalo, hivyo ameahidi kuwasisitiza wachezjai wake wakati wote watakapokua nchini Ufaransa wakiwania nafasi ya kuvuka kwenye hatua ya makundi.

Hata hivyo Hodgson amesema imeshawahi kutokea mwaka 1992, pale kikosi cha timu ya taifa ya Denmark kilipofanikiwa kutwaa ubingwa wa barani Ulaya na kuwashangaza wengi, jambo ambalo lilitokea baada ya timu hiyo kubezwa na kuonekana haiwezi.

“Imeaahi kutokea miaka ya nyuma na wenzetu waliweza, hivyo hata kwetu England naamini tunaweza kufanya jambo hilo.” Amesema Hodgson

Timu nyingine ambayo iliwahi kutwaa ubingwa wa barani Ulaya na kuwashangaza wengi, ilikua Ugiriki katika fainali za mwaka 2014 ambazo zilifanikiwa nchini Ureno.

Timu ya taifa ya England haijawahi kutwaa ubingwa wa barani Ulaya, tangu michuano hiyo ilipoanzishwa mwaka 1960.

Zlatan Ibrahimovic Awapa Masharti Man Utd
FA Yabaini Kulikua Na Kasoro Za Utovu Wa Nidhamu