Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Philip Mpango,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu ya Royal Tour jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka ametoa taarifa ya ujio wa uzinduzi wa Royal Tour  jijini Dodoma  wakati akizungumza na waandishi wa habari.

RC Mtaka amesema kuwa ujio huo ni baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuzindua filamu hiyo nchini Marekani na maeneo mengine nchini.

“Maandalizi yamekamilika kutakuwa jogging na burudani itayobebwa na utamaduni wa Dodoma ngoma za kigogo na kirangi,milango iko wazi kwa watakaopenda kujiunga na tukio hili,”amesema RC Mtaka

“Zao la zabibu linaongeza thamana ya yake kutoka kwenye wine kwenye mvinyo, tutakuwa na maonyesho ya mazao ya zabibu pia,”amesema

Amesema kuwa Ofisi yake imetoa fursa kwa baadhi ya Wilaya kuangalia tukio hili kupitia vyombo vya habari na utaratibu wote umekamilika.

Ikumbukwe kuwa mbali na Dodoma filamu ya Royal Tour ilianza kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huko nchini Marekani na hatimae jijini Arusha ,Zanzibar na Dar es Salaam.

Serikali kujikita na mapambano ya Ukatili kwa wanawake na watoto
Bernard Morrison aanika ukweli Simba SC