Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Salum Hamduni, amesema kuwa aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema, hajawahi kutoa taarifa kama anatishiwa maisha.

Kamanda Hamduni ameeleza hayo leo Novemba 9, 2020, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, baada kusambaa kwa taarifa kwamba Lema anashikiliwa nchini Kenya, alipokwenda kwa madai ya kutafuta hifadhi na bila kuwa na nyaraka muhimu.

Usalama wake hauko hatarini, yuko sawasawa tu na hakuna tishio lolote dhidi ya maisha yake, amesema Kamanda Hamduni.

Novemba 8, 2020, kulikuwa na taarifa kuwa Lema alishindwa kutoa nyaraka hizo muhimu kwa madai ya kuwa alikuwa anahofia maisha yake na kwamba alikuwa anaelekea nchini Kenya kwa ajili ya kutafuta hifadhi.

Lema aachiwa na polisi
Marais wa Urusi, Mexico wakataa kumpongeza Biden