Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Sweetbert Njewika, amekanusha kauli iliyodai kuwa amesema dereva bodaboda aliyeuwawa mkoani humo, hakuwa kiongozi wa CHADEMA na kusema kuwa alinukuliwa vibaya.

Akizungumza leo Februari 28, 2020 kamanda Njewike amesema kuwa walioitoa taarifa hiyo hawakumnukuu vizuri kwani yeye hakutoa taarifa ya moja kwa moja kuwa Alex Jonas hakuwa kiongozi wa CHADEMA.

“Nilichosema kwamba yule ni bodaboda inawezekana anafanya kazi nyingine, sikukanusha kwamba yule siyo kiongozi wa CHADEMA, naomba mninukuu vizuri na ndicho nilichokisema” amesema Kamanda Njewike.

Inadaiwa kuwa mwili wa Alex uliokotwa mbugani mbali na barabarani, ukiwa na majeraha ya kuchomwachomwa na kitu chenye ncha kali na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini nani aliyehusika na mauaji hayo.

Serikali yaagiza ardhi ya kilimo itengwe kwa vijana
Raia wa Afrika kusini waliopo China kurejea makwao

Comments

comments