Mwanafunzi Mack Rutherford (16) Raia wa Uingereza na Ubelgiji, ametua na ndege ndogo jijini Nairobi
nchini Kenya.

Rutherford ambaye ambaye yupo katika harakati za kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi Duniani kuruka peke yake kwa usafiri wa anga alianza safari akitokea jirani na mji mkuu wa Bulgaria Sofia Machi 2022 na anatazamia kuweka rekodi ya “Guinness World.”

Rekodi hiyo kwa sasa inashikiliwa na Travis Ludlow ambaye alikuwa na umri wa miaka 18 alipomaliza kuzunguka Dunia 2021.

“Kwanza nina furaha kufika hapa salama katika safari yangu na pia nataka kuwatia moyo vijana
wenzangu kufuata ndoto zao wasikate tamaa,” amesema Rutherford katika uwanja wa ndege wa
Wilson.

Akihojiwa na vyombo vya Habari mtengenezaji wa ndege hiyo Shark Aero amesema safari hiyo
ilikuwa ya hatari kwa Rutherford na kwamba tangu awali alikataa kushirikiana na mradi wake
unaohitaji ujasiri kuutekeleza.

“Anakuwa ni rubani kijana tena mwanamke mwenye umri mdogo zaidi kuruka peke yake duniani
na bila shaka atakuwa ni rubani mwenye ujuzi unaohitajika hapo baadae ingawa hatujisikii vizuri
kusukuma kikomo cha umri hadi kiwango cha chini kabisa cha safari,” amefafanua Aero.

Rutherford anatarajia kuzitembelea nchi nyingine nne za Afrika na Bahari ya Hindi kabla ya
kuelekea Mashariki ya Kati, Asia na Amerika Kaskazini na hatimaye kurejea tena Ulaya huku
akisema atalazimika kumudu changamoto zilizopo mbele yake.

“Mwonekano ulikuwa ni changamoto wakati wa kuruka jangwa la Sahara lakini mandhari
ilitosheleza na hali hiyo haijaniangusha ninalazimika kumudu vikwazo na pia nafurahia maoni ya
watu kwani yananijenga,” amesema.

Binti huyo anayetokea familia ya marubani alianza kumudu udhibiti wa ndege ya kwanza akiwa
na umri wa miaka saba chini ya uangalizi wa baba yake.

Akiwa na umri wa miaka 15 alikua ni rubani mwenye umri mdogo zaidi Duniani akirusha ndege
binafsi na sasa anafuata nyayo za dadake Zara ambaye alikuwa mwanamke mwenye umri mdogo
zaidi kuruka duniani kote na ndege akiwa na umri wa miaka 19.

Kauli ya Magufuli yajirudia kwa Samia
Rais Samia:Changamkieni fursa kwa kulinda miundombinu