Katibu Mkuu kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi amezindua mradi wa Kiuvuko cha kisiwa cha Rubondo MV kitakachokuwa kinafanya kazi ya kutoa huduma kwa Watalii watakokuwa wakifika kwa lengo la kutalii Hifadhi ya Kisiwa cha Rubondo.

Akizindua Kivuko hicho cha Rubondo MV, kitakachokuwa na uwezo wa kuchuua abiria 50 na Magari 6 kwa wakati mmoja na ambacho thamani yake ni shilingi Bilioni 2.3, amesema hatua hiyo itachangia kufikiwa kwa mpango wa maendeelo wa miaka mitano wa kuongeza idadi ya watalii.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu amesema hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha rubondo ni hifadhi maalum ya utalii kwa ajili ya utalii wa sokwe watu pamoja na utalii wa uvuvi hatua inayodaiwa itachagia kufikiwa kwa malengo ya idadai ya watalii kuongezeka kutoka walitii milioni moja mwaka 2016 hadi kufikia watalii milioni 2 kwa mwaka 2024 hadi 2025.

Raia wa Malawi wapiga kura za marudio kumchagua Rais
Mbaroni kwa kumtorosha na kumfanyia shambulio la aibu mtoto wa miaka 14