Msanii wa bongo fleva maarufu kama Ruby amemaliza tofauti alizokuwa nazo na Clouds Media Group, baada ya kuamua kumfuata Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa media hiyo, Ruge Mutahaba na kumuomba msamaha.

Mwanamuziki Ruby amekiri mapungufu yake na kusema kuwa hakuwa na haja ya kushindana na mzazi wake (Ruge) kwani siku zote mkubwa hakosei.

”Sikumbuki tarehe lakini i remember kama ilikuwa Oktoba, Novemba hivi. Nakumbuka nilikaa zangu tu nyumabani usiku kuna nafsi ikaniambia ”Ruby You need Piece” yule Ruge ni kama baba yako kwahiyo hata kama kwenye kazi watu tunakwaruzana zipo hizo tofauti ni kwamba jinsi ya kuzisolve, na kwa wakati ule hasira zilichukua nafasi yake kubwa sana kwahiyo mimi kama mimi nikasema No, Siwezi kushindana na mzazi” amesema Ruby.

Ambapo Fiesta ya mwaka 2015, Msanii Ruby hakuonekana Mwanza wala katika jukwaa la Fiesta wakati alikuwa mmoja wa wasanii waliosajiliwa akidai kuwa show hiyo alipangiwa kulipwa maslahi madogo kulinganisha na ukubwa wa tamasha.

Baada ya kukataa kushiriki katika tamasha hilo Clouds Media Group walisitisha kucheza nyimbo za mwanadada huyo na baada kuyaweka haya sawa sasa nyimbo za Ruby zitaanza kusikia katika media hiyo.

Yanga yatamba kuibuka kidedea dhidi ya Azam FC
Jeshi la Polisi lamjibu Dkt. Kigwangalla