Uongozi wa klabu ya AS Roma, umethibitisha taarifa za kutimuliwa kwa meneja kutoka nchini Ufaransa, Rudi Garcia ambaye msimu huu ameonekana kushindwa kwenda sambamba na ushindani katika ligi ya nchini Italia.

AS Roma walianza kuhusishwa na mipango ya kuwa mbioni kumtimua Rudi Garcia, Tangu juma lililopita baada ya kikosi chao kukubali kulazimishwa matokeo ya sare ya bao moja kwa moja dhidi ya AC Milan.

Msukumo mkubwa wa kutimuliwa kwa meneja huyo mwenye umri wa 51, pia umechangiwa na upinzani mkali uliopo kwenye msimamo wa ligi ya nchini Italia Sirie A, ambapo inaonekana kuna tofauti ya point saba kati ya AS Roma dhidi ya vinara SSC Napoli.

Luciano Spalletti

Tayari taarifa zinadai kwamba huenda AS Roma wakamrejesha Luciano Spalletti ambaye aliwahi kuwa meneja klabuni hapo kuanzia mwaka 2005–2009.

Spalletti ambaye alipoteza kibarua chake huko nchini Urusi alipokua akikinoa kikosi cha FC Zenit Saint Petersburg, amekua pembeni ya tasnia ya ufundishaji wa soka tangu mwezi Machi mwaka 2014.

Hata hivyo anaaminiwa huenda akaleta mabadiliko kwenye kikosi cha AS Roma ambacho kinahitaji usaidizi wa kurejesha hadhi yake ya ushindani katika ligio ya nchini Italia hadi kufikia malengo ya kutwaa ubingwa.

Kwa sasa AS Roma wanashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ya nchini Italia (Sirie A) kwa kufikisha point 34.

Saad Kawemba: Bado Tutaendelea Kuutumia Uwanja Wetu CAF
Stand United Na Simba Zatozwa Faini